Burkina Faso Tafuta Vyama Vyote vya Siasa

Serikali ya Burkinabe imefuta rasmi Vyama na Mashirika yote ya Kisiasa nchini humo Mamlaka ikisema uamuzi huo ni hatua kuu katika ujenzi wa Serikali, ndani ya mfumo wa mpito unaoendelea tangu Mapinduzi ya 2022.

Baraza la Mawaziri la Burkina Faso limebainisha kuwa kuenea kwa Vyama vya Siasa, vinakuza mgawanyiko kati ya raia na kudhoofisha mfumo wa kijamii.

Shughuli za Vyama vya Siasa tayari zilikuwa zimesitishwa tangu Septemba 2022, kufuatia kuingia madarakani kwa Kapteni Ibrahim Traoré baada ya Mapinduzi yaliyompindua Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba.

Akiwasilisha amri hiyo mwishoni mwa Baraza la Mawaziri, Waziri wa Utawala, Émile Zerbo, pia alitangaza kupitishwa kwa Muswada wa kufuta makubaliano yanayosimamia uendeshaji na ufadhili wa Vyama vya Siasa.

Related Posts