Nature

CCM Wajibu Madai ya Kusomba Watu na Mabasi Kwenda Kwenye Mikutano ya Kampeni

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohamed, amesema kuwa madai ya baadhi ya watu kwamba chama hicho kinasomba watu kwa mabasi kwenda kwenye mikutano yake ni hoja dhaifu na isiyo na mashiko kisiasa.

Akizungumza Jumanne, Septemba 2, 2025, Jijini Dodoma wakati akitoa tathmini ya kampeni za siku sita za chama hicho, Jawadu amesema hakuna ubaya wowote katika kuwasafirisha wanachama au wafuasi kwenda kwenye mikutano ya kisiasa.

Ameeleza kuwa katika sayansi ya siasa, njia yoyote halali inayotumiwa na chama kufikia umma ili kupata uungwaji mkono ni uamuzi wa chama husika, na si jambo la ajabu kwa CCM kuwasaidia wanachama wake kusafiri kwa ajili ya kushiriki mikutano.

Amehitimisha kwa kusema kuwa mikakati ya chama hicho inalenga kuhakikisha wananchi wanapata ustawi bora wa maisha, hivyo kusaidia usafiri kwa baadhi ya wanachama ni sehemu ya kujenga mshikamano na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za chama.

Related Posts