Dakika nane alizocheza beki Attohoula Yao zimetosha kumtoa chozi daktari wa viungo wa Yanga SC, Youssef Ammar aliyedai kuwa haikuwa rahisi kumrudisha uwanjani na anamuona akirudi kwa ubora mkubwa.
Yao ambaye amekaa nje zaidi ya miezi saba, alipata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya TRA United akiingia dakika ya 82 kuchukua nafasi ya Kibwana Shomari kwenye Kombe la Mapinduzi juzi.
Akizungumza na Mwanaspoti, Youssef alisema amefurahishwa na dakika chache alizozipata Yao baada ya kuwa nje ya uwanja muda mrefu akiuguza jeraha la goti.
Mwanaspoti
