Nature
Diva Atangaza Kuwashtaki Crown Media Kwa Kumchafua na Kumdhalilisha

Diva Atangaza Kuwashtaki Crown Media Kwa Kumchafua na Kumdhalilisha

Crown Media ,Ninaandika barua hii rasmi kuhusiana na kitendo cha kunidhalilisha na kunichafua kilichofanywa na Crown Media kupitia mahojiano na Gift Stanford yaliyotangazwa kwenye kituo chenu.
Kauli na maudhui yaliyotolewa katika mahojiano hayo yalikuwa na taarifa za uongo, zisizo na ushahidi na zenye madhara makubwa kwa heshima, taswira na sifa yangu binafsi na kitaaluma nia yenu ni views na comment na content ambayo kiuhalisia ni kosa kisheria , Kama Media Personality lakini Pia Business woman hii haikubaliki

Mahojiano haya yalifanyika na kurushwa bila uangalizi wa kitaaluma, bila kuthibitisha ukweli wa taarifa toka hospitali na evidence tena mtangazaji alikuwa very comfortable 1 na zaid yalikuwa mazungumzo ambayo hayakuwa na balance of the story ambayo imekiuka miiko ya uandishi wa habari na zaid bila kuzingatia maadili ya taaluma ya habari, jambo lililosababisha kudhalilishwa hadharani na kuathirika kwa heshima yangu. Matendo haya yamesababisha maumivu ya kisaikolojia, kupoteza imani kwa jamii, na hasara ya kitaaluma.
Kwa msingi huo, ninaitaka Crown Media:

  1. Kutoa msamaha wa hadharani kwangu kupitia majukwaa yote yaliyotumika kusambaza maudhui hayo (ikiwemo televisheni, redio, tovuti na mitandao yenu ya kijamii). Msamaha huo uwe wa wazi, wa dhati na utakao kubali madhara yaliyosababishwa.
  2. Kuondoa maudhui yote yenye kunidhalilisha kutoka kwenye majukwaa yenu, ikiwemo mahojiano yote na vipande vyake vilivyotumika kama matangazo.
    Nawaarifu kuwa endapo mtaacha kutekeleza matakwa haya ndani ya siku 7 tangu tarehe ya barua hii, sitakuwa na budi kuendelea na hatua za kisheria dhidi ya Crown Media, kipindi husika na mtangazaji aliyehusika, nikidai fidia kwa madhara ya kashfa na udhalilishaji uliofanywa.
    Barua hii inatumika kama taarifa rasmi ya wito wa kuomba msamaha na pia taarifa ya nia ya kushtaki. Natarajia Crown Media itachukulia jambo hili kwa uzito unaostahili na kuchukua hatua haraka kurekebisha

tayari Pia kuhusu Presenter nimewasilisha malalamiko yangu kisheria @ithibatitz
lakini ni juzi tu tcra walileta #Futakabisa ikiwa ni kosa kusambaza habari zisizo na uhakika , I am taking legal action kwa Hii Media as well for defamation

Related Posts