Donald Trump Amshambulia Papa Leo XIV Kwa Kauli Kali

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa kauli kali dhidi ya Pope Leo XIV, akimtuhumu kuwa “dhaifu katika masuala ya uhalifu” na “mbaya katika sera za mambo ya nje.”

Kauli hiyo ilitolewa baada ya Papa Leo XIV kutoa wito wa amani na kukemea vita pamoja na matumizi ya lugha ya vitisho kuhusu mgogoro wa Iran.

Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii, Trump alisema:
“Papa Leo ni dhaifu katika kupambana na uhalifu, na ni mbaya kwa sera za mambo ya nje.”

Trump pia alimkosoa Papa kwa kile alichodai kuwa ni msimamo laini kuhusu Iran na sera za uhamiaji, jambo lililoibua mjadala mkubwa kati ya viongozi wa kisiasa na wa dini duniani.

Mvutano huu unaonyesha tofauti kubwa ya mitazamo kati ya Ikulu ya Marekani na Vatican kuhusu vita, diplomasia, na masuala ya kibinadamu.

Related Posts