Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) linajiandaa kufanya droo ya raundi ya awali ya ligi ya mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa Msimu wa 2025/2026.
Tukio Hilo Litafanyika katika Mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salam .Kwa mujibu wa tovuti ya Qatari ya WinWin, Hafla hiyo Imepangwa kufanyika
Agosti 09 Saa 8 Mchana kwa Saa za Tanzania.
Yanga na Simba zitaiwakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa huku Azam FC na Singida Black Stars wakiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho.

