Baada ya Majizo kutoa taarifa kuwa anaomba msamaha kwa niaba ya wasanii, baadhi ya wasanii wameonyesha kuchikizwa na kitendo hicho na kuomba awatoe katika watu ambao wameomba msamaha huo.
Dulla Makabila ✍
Boss @majizzo Kwanza Asante Kwa Kutuwazia Mema Wadogo Zako Ila Mimi Nataka Nikuombe Tu Unitoe Kwenye Watu Ambao Unawaombea Msamaha Kwa Sababu Eti Ya Kuwakela Watu Kutokana Na Maisha Yao Mzee Binafsi Kipindi Najitafuta Kimaisha Nilishawahi Kutupiwa Vitu Vyangu Nje Na Mwenye Nyumba Na Nikafukuzwa Kama Mbwa Na Watu Waliona Na Wenye Kucheka Walicheka Sasa Leo Kuna Ubaya Gani Walionicheka Wakiona Nimenunua Gari Tatu Kwa Pamoja Sio Hao Tu Na Kuna Watu Naishi Nao Kwenye Tasnia Na Najua Hawanipendi Wamejificha Kwenye Kivuri Cha Urafiki Huku Wakipambana Kwa Siri Kuniua Kimziki Kwa Kutumia Wasanii Wengine Uzuri Nawajua Na Nacheka Nao Kama Sijui Vile
Hivo Basi Maisha Yangu Kama Yanawakela Ndio Lengo Langu Mzee Kwa Sababu Sina Mpango Wa Kuacha Leo Wala Kesho Kuwakera Mpaka Ukiona Mungu Amenipa Riziki Ya Kununua Gari Tatu Kwa Pamoja Maana Yake Anajua Nilipitia Kipindi Gani Na Ameridhika Hao Watu Wapitie Hizi Kero
Kimsingi Kwa Mimi Ungeniacha Tu Niendelee Kuwakela Sababu Ndio Maisha Niliyochagua Nna Miaka Zaidi Ya Kumi Kwenye Singeli Sijawahi Kusainiwa Kwenye record label yeyote Wala Sijawahi Kuwa Boss Ambae Anawekeza Ata 2000 Kwenye Mziki Wangu Kuanzia Audio Zangu Video Kodi Gari Nazomiliki Gharama Za Vifaa Vya Kufanyia Makafala Na Kodi Nazowalipia Wanawake Zangu Hela Nazofanya Matumizi Zote Zinatoka Mfukoni Kwangu Maana Yake Ata Mimi Nikiwa Na 5000 Maana Yake Kampuni ina 5000 Sina Naemtegemea Ndio Maana Ukinikataza Kuwakela Kwa Mafanikio Ambayo Nimeyapambania Wewe Ndio Unanikera Mimi Naomba Niache Mzee Majjizo Ukizidisha Sana Ushauri Ntakuimba 😡😡😡😡
LA MWISHO SHABIKI WA KWELI HAWEZI KUCHUKIZWA NA MAFANIKIO YANGU AKICHUKIA MAANA YAKE ANANICHUKIA SIO SHABIKI YANGU SHABIKI YANGU LAZIMA NAPOFURAHI YEYE AFURAHI MARA MBILI YANGU
SOON NAACHIA WIMBO ALAFU NIWAONE MSIANGALIE MAANA HAKUNA MWENYE UWEZO WA KUSHINDANA NA MITISHAMBA 💪
CALL ME 👑🎤
