EDO Kumwembe Auliza Swali Gumu “Kwanini Mangungu Asiwaachie Simba Timu Yao”

Ameandika Edo Kumwembe;

Nina mawili tu…sina mengi. Kuhusu hili la Murtaza. Simba angeingia kipindi cha pili, akaongeza bao la tatu au Kante asingerudisha pasi fupi kwa kipa Esparance wasipate bao na mpira ukaisha kusingekuwa na maandamano na vurugu kuhusu Murtaza. Wangesifiwa wachezaji na kocha wao. Napenda siku moja maandamano haya yaje wakati Simba ikiwa ina matokeo mazuri. Kwanini timu ikifungwa inakuwa ya Mangungu na ikishinda inakuwa ya wachezaji na kocha na MO?….jambo la pili. Kama mimi ningekuwa Mangungu, kwanini nisiwaachie Simba timu yao? Mangungu ni msomi na hana dhiki ya visenti. Sidhani kama Simba inamnufaisha kiuchumi. Angewaachia tu Simba yao akafanya mambo yake. Inafika mahala nadhani anaisononesha hata familia yake. Haijalishi yupo sahihi au hayupo sahihi inafika muda unaachana na kila kitu. Muda utaamua kama yeye alikuwa tatizo au sio……

LEGEND

Related Posts