Nature

Edo Kumwembe: Binafsi Naamini Almasi Kasongo na Steven Mguto Wametolewa Kafara

Edo Kumwembe: Binafsi Naamini Almasi Kasongo na Steven Mguto Wametolewa Kafara

EDO KUMWEMBE amesema kuwa “Tunaahirisha mechi bila ya kujua madhara yake. Kuna watu wanaingia gharama nyingi kutoka mikoani kuja kutazama mechi. Watu wanatoka Simiyu, Newala, Ngara na kwingineko kuja kuangalia dabi. Wanatumia mamilioni ya pesa kwa nauli na kuja kukaa katika nyumba za kulala wageni. Lakini ghafla simu moja kutoka juu inaamua kuahirisha mechi.

Kampuni ya Azam TV iliyotia mamilioni ya pesa kama udhamini katika ligi yetu inaingia hasara kubwa kwa kutoonyesha pambano hilo kwa sababu ya simu ya mtu mmoja tu kutoka juu. Upuuzi wa karne nyingi zilizopita.

Kuna wadhamini wa Ligi ambao kupitia mechi kama hii wanapata fursa kubwa ya kujitangaza, lakini mtu mmoja anapiga simu kutoka juu na kuahirisha pambano kwa sababu zake binafsi. Kampuni zikijitoa katika udhamini klabu zinapata shida kujiendesha.

Watu wa Bodi wawe imara, lakini kwa wakubwa ambao wanaingilia mechi hizi kwa maslahi yao nadhani wanapaswa kupata funzo kubwa kwa kilichotokea. Binafsi naamini Almasi Kasongo na Steven Mguto wametolewa kafara tu katika sakata hili. 📌

Kuna mtu ametulia sehemu kama kivuli akishuhudia kung’olewa kwa Mnguto na Kasongo, lakini anajua kwamba yeye ndiye chanzo cha pambano hili kutochezwa. Mtu huyu naye tumwambie ‘never again’ na asiharibu mpira wa nchi hii.

Fifa hawakuwa wajinga kutaka mpira wa miguu ujitegemee. Walijua kwamba kuna aina ya watu wataleta utata mkubwa kama huu.

Tusipokemea itajirudia tena na tena. Tutaendelea kuwatoa kafara watu wengi wasiohusika

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *