Nature

Ester Bulaya Afunguka Sababu za Kurudi CCM

Kada wa zamani wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema anayejulikana kwa majina ya Ester Bulaya ametema nyongo ikiwa ni siku chache tu mara baada ya kuhamia katika Chama Cha Mapinduzi yaani CCM.

Siku chache zilizopita Ester Bulaya alitangaza nia yake ya wazi ya kutaka kuhamia katika CCM na mpaka sasa tayari amechukua fomu ya kugombea ubunge chini ya mwamvuli wa chama hicho kikongwe na chenye historia bora kwenye masuala ya siasa nchini.

Ester Bulaya mara baada ya kukamilisha mchakato wake wa kuhamia CCM, ameibuka hadharani na kueleza kwamba Chadema kwa sasa wameshuka daraja na hawana hali ya upinzani tena na ndio maana hakuona sababu ya kuendelea kubaki kule.

Ester katika taarifa aliyoitoa siku ya jana Jumatatu 30 Juni, alieleza wazi kwamba hapo awali yeye alikuwa ni kada kindakindaki wa CCM kabla ya kuhamia Chadema mwaka 2015 hivyo basi ni kama alienda uko kwa mkopo na baada ya chama hicho kushuka daraja (kususia uchaguzi), ameamua kurudi kwenye chama chake cha mwanzo.

Katika uhalisia tunaweza kueleza kwamba moja kati ya sababu zilizomtoa Bulaya Chadema ni suala la chama hicho kujiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu kutokana na kampeni yao inayoeleza kwamba No Reforms, No Election.

Chadema mpaka sasa ni kama wameainisha wazi kwamba hawatashiriki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu mpaka pale mabadiliko ya katiba yatakapofanywa na chama tawala yaani CCM.

Msimamo huu wa chama ndio unaotajwa kama sababu ya kuendelea kuwagawa wanachama wa chama hicho ambapo mpaka sasa wengi wao wameamua kuhamia CCM kwani wanaamini wakiwa watapata haki yao ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *