Nature

Familia Yadhibitisha Kifo Cha MC Pilipili Kimesababishwa na Kipigo

Kaka wa marehemu Emmanuel Mathias, maarufu kama MC Pilipili, Christopher Matebe amesema matokeo ya uchunguzi wa awali yameonyesha kwamba kifo cha mdogo wake kilisababishwa na kupigwa na watu wasiojulikana hii ni baada ya Mwili wake kukutwa na majeraha

Kaka wa MC Pilipili ameyasema hayo hii leo wakati akitoa Mrejesho wa awali juu ya Uchunguzi unao endelea ambapo ameushukuru uongozi wa Hospitali ya General pamoja na Mbunge wa Dodoma Mjini Antony Mavunde kwa kuwa karibu na familia katika kipindi hiki kigumu na amesema kuwa shughuli za kumuaga zinaendelea nyumbani kwao na ibada ya maziko itafanyika nyumbani kwao Swaswa Dodoma na amesisitiza taratibu za Uchunguzi ameliachia Mamlaka za Serikali.

Related Posts