FIFA Yakataa Ombi la IRAN Kuhamisha Mechi zake za Kombe la Dunia Kutoka Marekani

FIFA imeripotiwa kukataa pendekezo la Iran la kuhamisha mechi zake za Kombe la Dunia 2026 kutoka Marekani hadi Mexico.

Ombi hilo limekuja baada ya Maofisa wa Iran kuibua wasiwasi wa kiusalama na kueleza upendeleo wa kuepuka kucheza kwenye ardhi ya Marekani huku kukiwa na mvutano wa kisiasa wa kijiografia.

Licha ya kutokuwa na uhakika juu ya ushiriki, Iran hatimaye ilithibitisha kwamba bado ina nia ya kushiriki katika Mashindano hayo.

Kwa mujibu wa habari, FIFA haina mpango wa kubadilisha Viwanja vilivyopangwa vya Los Angeles na Seattle. Maofisa wanaamini kuwa hatua kama hiyo haitawezekana kwa kuwa tiketi tayari zimeuzwa na kubadilisha maeneo kutaleta matatizo ya kiufundi kwa timu nyingine kwenye kundi.

Iran italazimika kucheza mechi zake huko Merekani kama ilivyopangwa hapo awali.

Related Posts