Nature

Gari la Mgombea Urais CHAUMMA Salum Mwalim Lachomwa Moto

Gari analotumia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA) Salum Mwalim, limepigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa jiwe kwenye kioo cha nyuma na Mtu asiyejulikana muda mfupi baada ya kumshusha Mgombea huyo hotelini Mafinga, Mkoani Iringa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Taarifa kwa Umma wa CHAUMMA John Mrema amesema tukio hilo limetokea usiku wa jana Septemba 29, 2025 wakati Mwalim aliposhushwa hotelini kwa ajili ya kupumzika na gari hilo walitoka nalo wasaidizi na walipofika nje kitu kinachodhaniwa kuwa ni jiwe kilipiga gari hilo.

“wakati gari yake inatoka kwa ajili ya wasaidizi wake kwenda kutafuta vyumba karibu na hoteli yake kabisa gari yake ikashambuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni jiwe na kuvunja kioo cha nyuma”

Kwa mujibu wa Mrema watu wanne wanaodhaniwa kuwa wametekeleza tukio hilo wamekamatwa. Huku akisema kuwa wamewaachia polisi jambo hilo.
1h

Related Posts