Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kiwango bora kilichoonyeshwa na mchezaji wa timu ya Taifa Stars, Ibrahim Bacca kimempa umaarufu duniani.
Msigwa ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Januari 10, 2026, wakati wa hafla ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuipongeza timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, pamoja na wanamichezo wengine inayofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
“Huyu ni Sanjenti wa KMKM, alimkaba yule Osimhen anayecheza Galatasary mpaka akakasirika akatolewa na hakufunga na Bacca amekuwa maarufu dunia nzima,” amesema.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), benchi la ufundi, wachezaji wa Taifa Stars pamoja na wadau wa michezo
