Godbless Lema “Msiende Kwenye Show Wanazo Tangaza Wasanii Machawa”

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo @chadematzofficial Godbless Lema @godblessjlema1 ametoa wito kwa Gen-Z kutokushiriki katika jambo lolole linalowahusu wasanii akiwaita ‘chawa’ akisema kuwa ni wakati wa kuwapiga ‘ban’.

Katika andiko lake alilochapisha katika mtandao wa Instagram Lema amesema hata ikitokea wametangaza show wasiende, miziki wanayoweka kwenye majukwaa mbalimbali wasisikilize.

Pamoja na hayo ametaka yata mahojiano watakayofanyiwa wasisikilize pamoja na hata tuzo watakazoteuliwa wasipigiwe kura.

Hii inakuja siku chache baada ya Mmiliki wa vituo vya EFM na TVE Francis Sciza (Majizzo) kuwaombea wasanii msamaha kwa mashabiki baada ya kutokuwepo kwa kuungwa mkono kwa wasanii hao.

Upi mtazamo wako.

Related Posts