Nature

Hasira za GEN Z Laitikisa Taifa, Rais Adai Wametumwa Kumpindua

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, leo Ijumaa ameshutumu kile alichokitaja kuwa jaribio la kupindua serikali yake, baada ya siku kadhaa za maandamano makubwa yanayoongozwa na vijana maarufu kama “Gen Z”.

Maandamano hayo, yaliyoshika kasi tangu Septemba 25 mjini Antananarivo, yamechochewa na uhaba wa maji na umeme na sasa yameenea katika maeneo mengine ya nchi. Waandamanaji wanamtaka Rajoelina kujiuzulu, wakipinga kile wanachokiita miaka mingi ya utawala mbaya na upendeleo wa kisiasa.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 51 amevunja baraza lake la mawaziri na kuahidi kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kurejesha utulivu. Hata hivyo, amewashutumu waandamanaji kwa kutumiwa na watu wenye maslahi binafsi kuchochea mapinduzi, akionya kuwa lengo lao ni “kuharibu nchi.”

Related Posts