Bondia @hassanmwakinyojr ametangaza kurejea nafasi ya kwanza barani Afrika (middle) na kushika nafasi ya 37 duniani kati ya mabondia 1,950 kwa mujibu wa viwango vipya vya ubora duniani (Boxing Record).
Kupitia ujumbe aliouandika kwa maneno makali, Mwakinyo amesema ushindi wake dhidi ya bondia aliyemuita “mlemvi” na asiye kuwa “level” yake umemrejesha kwenye nafasi yake ya heshima na kutuma ujumbe kwa wapotoshaji kwenye tasnia ya masumbwi.
“Niko hapa kuwajulisha ya kwamba yule bondia mlemvi ambaye hakua level yangu amenirudisha tena kuwa top namba moja AFRICA na no 37 kati ya mabondia 1,950,” ameandika Mwakinyo.
Mwakinyo amesisitiza kuwa licha ya kutokuwa na ulazima wa kujisifia, ameamua kuweka wazi mafanikio yake kutokana na kuwepo kwa mabondia “wenye makengeza” na wanaopotosha tasnia. Amehitimisha kwa kusema, “Mapovu ruksa.”
