
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Bi Alice Haule, mjane wa marehemu Justice Rugaibula, amevamiwa kwenye nyumba yake (Nyumba namba 3) iliyoko Tembo Street, Mikocheni Bakharesa, jijini Dar es Salaam na watu aliodai kuwa wametumwa na mmoja wa wafanyabiashara ambaye kwa muda mrefu wamekuwa ‘wakivutana’ kisheria Mahakamani kwa kesi tofauti za madai, hata kabla ya mumewe kufariki
Taarifa kutoka kwa familia hiyo ilizozipata Jambo TV kutoka kwa mtoto wa mama huyo aitwaye Grace Justice Rugaibula zimeeleza kuwa uvamizi huo umefanyika asubuhi ya leo, Jumanne Septemba 23.2025 ambapo watu hao walifika kwenye geti la nyumba hiyo ambayo kwa sasa imepangishwa kwa raia wa Kichina na kuvunja geti, kabla ya kuingia ndani na kuanza kuwashambulia watu waliokuwa ndani sambamba na kuanza kutoa vitu nje kinyume na taratibu
Familia hiyo inasema inatambua kuwa mfanyabiahara anayedaiwa kuwatuma watu hao miaka ya nyuma alikuwa na ushirikiano wa kibiashara na marehemu Justice Rugaibula, ambapo marehemu alikopa kiasi cha shilingi millioni 150 kutoka kwake, lakini fedha hiyo ililipwa hata kabla ya kifo chake, lakini walishangazwa kuona ghafla anaibuka na kudai kuwa nyumba hiyo ameuziwa
Grace Justice Rugaibula amesema jambo hilo limepelekea familia kufungua kesi mbili moja ya kudai hati ya nyumba yao na nyingine ya kupinga kughushiwa kwa saini ya Bi Alice Haule

