Nature

Inasikitisha, DUNIA Imeshindwa Kuwatetea Wapalestina, Waendelea Kuteseka

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameikemea vikali jumuiya ya kimataifa kwa kile alichokiita “kutochukua hatua” huku maelfu ya Wapalestina wakiendelea kuteseka katika Ukanda wa Gaza.

Akiwasilisha ujumbe wake kwa njia ya video katika mkutano wa kimataifa wa shirika la Amnesty International, Guterres amesema hali inayoshuhudiwa Gaza ni “mgogoro wa kimaadili unaopima dhamira ya dunia nzima”, huku akisisitiza kuwa mateso ya binadamu yamefikia kiwango kisichokubalika tena.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya Wapalestina 1,000 wameuawa tangu Mei 27 wakiwa katika harakati za kutafuta chakula.

“Dunia iko katika vita vya kimataifa vya utu wa binadamu kwa ajili ya haki za binadamu na haki. Siwezi kueleza kiwango cha kutojali tunachokiona – ukosefu wa huruma, ukosefu wa ukweli, ukosefu wa ubinadamu,” alisema Guterres kwa masikitiko makubwa.

Kauli yake imekuja wakati ambapo mashirika ya misaada ya kibinadamu yanaendelea kutoa onyo kuhusu hali mbaya ya kibinadamu Gaza, huku raia wa kawaida wakiendelea kulengwa na ukosefu wa misaada muhimu, chakula, na huduma za afya.

Amnesty International na mashirika mengine ya haki za binadamu yamekuwa yakitaka hatua madhubuti zichukuliwe kuwalinda raia na kuzuia ukiukwaji wa haki katika mzozo huo.

Related Posts