Kazi ya uokoaji imekamilika katika Mji wa Ahmeddabad ilikotokea ajali ya Ndege nchini India lakini Wachunguzi wanaendelea kuitafuta miili ya watu na ushahidi mwingine.
Watu zaidi ya 240 wamefariki kwenye ajali hiyo iliyohusisha ndege aina ya Boeing 787 ya Shirika la Ndege la India.
Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kwamba India inafikiria kusitisha matumizi ya Ndege hizo kwa ajili ya kuzifanyia ukaguzi wa usalama wa Ndege hizo.
Aidha Waziri mkuu wa India Narendra Modi ametembelea hii leo katika jimbo la Gujarat, eneo ilikotokea ajali hiyo ambako ni nyumbani kwa Waziri mkuu huyo.
Mtu pekee aliyenusurika kati ya Watu 242 waliokuwemo ndani ya Ndege hiyo ya abiria iliyokuwa ikielekea London amesema hata yeye anashangaa jinsi alivyonusurika kimuujiza katika ajali hiyo ya Ndege.

