INEC Yateua Mbunge Viti Maalumu Kuziba Nafasi ya Marehemu Halima Nassor

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake kilichofanyika leo Januari 30, 2026 imefanya uteuzi wa Ndugu. Beng’i Mazana Issa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Hlalima Idd Nassor, wa CCM aliyefariki tarehe 18 Januri 2026.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi waTume hiyo, Kailima Ramadhani, imesema uteuzi huo wa Beng’i Issa, umezingatia masharti ya Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 112 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani, Sura ya 343,

Aidha, taarifa hiyo imesema kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 25(1)(c) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288 kikisomwa pamoja na kifungu cha 113 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya 343, Tume katika kikao hicho imefanya uteuzi wa Ndugu Irene Linus Mwangara wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kuwa Diwani wa Viti Maalumu katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Uteuzi huo umefanyika baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa marudio katika kata ya Mzinga, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo uchaguzi uliahirishwa kutokana na kifo cha mgombea katika kata husika.

Related Posts