IRAN Wamesisitiza Hakuma Mtu wa Kuwazuia Kucheza Kombe la Dunia

Kwa kifupi tu ni kwamba , Shirikisho la Soka la Iran (FFIRI) limepinga kauli ya Donald Trump kuhusu kushiriki kwa timu ya taifa ya Iran kwenye Kombe la Dunia 2026.

FFIRI imesema Kombe la Dunia ni tukio la kimataifa na linasimamiwa na FIFA, siyo nchi yoyote au mtu binafsi. Wameongeza kuwa Iran ni miongoni mwa timu za kwanza kufuzu kwa Kombe hilo na hakuna anayeweza kuwazuia kushiriki

Ikumbukwe siku kadhaa nyuma Trump alisema ingewezekana si salama kwa timu ya Iran kushiriki Kombe la Dunia nchini Marekani kutokana na hali ya kisiasa kati ya Marekani na Iran.

Hata hivyo baadae Rais wa FIFA, Gianni Infantino, alisema kuwa Trump alimhakikishia kuwa timu ya Iran inakaribishwa kushiriki

Related Posts