
Iran kupitia Vyombo vya habari vya nchi hiyo, imekiri rasmi kwamba Ali Larijani, Mkuu wa Baraza la Taifa la Usalama (Supreme National Security Council), ameuawa.
Hii ni mara ya kwanza Serikali ya Tehran kukiri kifo chake baada ya ripoti za awali.
Ripoti za Kimataifa zinasema Larijani aliuawa katika shambulio la anga lililotekelezwa na Jeshi la Israel dhidi ya maeneo ya Tehran na miji jirani.
Ali Larijani alikuwa Mtendaji muhimu wa siasa na usalama wa Iran kwa miongo kadhaa. Alishika nyadhifa mbalimbali za juu, akiwemo kama Spika wa Baraza la Wawakilishi na kisha kiongozi wa Baraza la Taifa la Usalama, kazi ambayo ilimfanya awe miongoni mwa wanaume wenye ushawishi mkubwa katika siasa za Iran.
Kifo chake kinakuja wakati wa mzozo mkubwa wa kivita kati ya Iran na Israel, na ni mojawapo ya vifo vya kimkakati vinavyoathiri muundo wa Uongozi wa Tehran.
