Jakaya Kikwete: Ridhiwani Kupita Bila Kupingwa ni Kawaida

Jakaya Kikwete: Ridhiwani Kupita Bila Kupingwa ni Kawaida

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kupita bila kupingwa kwa Mgombea wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete si jambo la ajabu imekuwa ni kawaida kutokana na Wilaya ya Bagamoyo kuwa na Wingi wa Wananchama wa CCM.

Kikwete ameyasema haya leo Julai 31, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Viwanda Kwala, Kibaha mkoani Pwani ambapo Mgeni Rasmi amekuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, ameongeza kuwa hata katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na 2015 pia Ridhiwani Kikwete alipita bila kupingwa akiwa ni Mgombea pekee ndani ya Chama hicho cha CCM.

Related Posts