Dar es Salaam, Tanzania Kupitia ukurasa wake wa Instagram Instastory Jesca Magufuli Jesca Magufuli ametoa taarifa kwa umma kuhusu akaunti zisizo rasmi zinazotumia jina lake kwenye mtandao wa Facebook.
Amesema, Ningependa kuufahamisha umma kuwa mimi sina akaunti ya Facebook yenye jina Jesca Magufuli. Akaunti zote zinazoonekana kwenye Facebook kwa jina hilo si zangu na zinatumiwa bila idhini yangu. Pia, akaunti hizo zinatumika kutapeli watu.
Jesca Magufuli amewaomba wananchi kupuuza taarifa zote zinazochapishwa kupitia majina hayo, akisisitiza kwamba kutumia utambulisho wa mtu mwingine mtandaoni ni kosa kisheria. Amesema Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act, 2015), kifungu cha 15, kinakataza mtu kuiga au kutumia utambulisho wa mwingine kupitia mfumo wa kompyuta au mtandao. Aidha, kifungu cha 305 cha Sheria ya Jinai ya Tanzania (Penal Code) kinaeleza kuhusu udanganyifu (false pretences) na madhara yake.
Taarifa hii inakuja kama tahadhari kwa wananchi dhidi ya akaunti zisizo rasmi zinazoweza kusababisha udanganyifu au utapeli mtandaoni. Jesca Magufuli amesisitiza umuhimu wa uhakika na tahadhari wanapotumia mitandao ya kijamii.

