Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeonesha kutoridhishwa kwake na uamuzi wa Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kukataa kujitoa katika shauri linalohusu mgogoro wa ndani wa chama hicho kuhusu usimamizi na mgawanyo wa rasilimali zake, likielezwa kuwa uamuzi huo unaashiria kile ilichokiita kiburi cha kimahakama na upendeleo kwa upande wa walalamikaji.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatatu Julai 28, 2025, mara baada ya kesi hiyo kusikilizwa jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema kuwa maamuzi ya jaji huyo yanaonesha bayana kuwa haki inacheleweshwa kwa makusudi,
Kwa mujibu wa Mnyika, licha ya jaji kueleza kuwa ana ratiba ngumu ya kazi na kushindwa kupata muda wa kutosha wa kusikiliza kesi hiyo kwa haraka, bado ameendelea kushikilia shauri hilo, jambo alilolitafsiri kuwa ni njama ya kuhakikisha upande mwingine haupati haki kwa wakati

