
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imependekeza adhabu ya kifo kwa Rais wa zamani Joseph Kabila kwa tuhuma zikiwemo za Uhaini na uhusiano na kundi la Wanamgambo wa AFC/M23.
Anatuhumiwa kwa uhalifu wa Kivita, uhalifu wa kutumia nguvu kama Kiongozi wa M23 na njama ya kujaribu kufanya Mapinduzi.
Mwendesha Mashtaka pia ameomba mali zake zote zikamatwe.
Kabila, ambaye hakuhudhuria kesi hiyo, hakuzungumza mara moja hadharani kuhusu hukumu ya kifo.
Kabila (54), alitawala DRC kwa miaka 18 kuanzia 2001.
