Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa tamko kali kufuatia kuenea kwa taarifa na mijadala mitandaoni inayolihusisha jeshi hilo na masuala ya kisiasa, likionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa leo jijini Dodoma na msemaji wa JWTZ, Kanali Gaudentius Ilonda, jeshi limesema limeanza kufuatilia kwa karibu watu na kurasa za mitandao ya kijamii zinazojihusisha na kusambaza taarifa zenye lengo la kulichafua au kulipotosha jeshi hilo mbele ya umma.

