Rais wa Rwanda ametupilia madai ya kumuandaa Mtoto wake kuwa mrithi wa kiti cha Urais atakapoondoka Madarakani.
Akizungumza mjini Kigali amesema kuwa Watoto wake ni Wanyarwanda sawa na wengine ambao wanapaswa kuishi maisha ya kawaida.
Rais Kagame ameweka wazi kuwa hawezi kumtafutia mtu Urais na kuthibitisha kuwa hata Mtoto wake wa kike wanayemtaja kuandaliwa kuchukua Madaraka huenda hataki.
Rais huyo wa Rwanda amekuwa Madarakani kwa miaka kadhaa akiendelea kuijenga nchi hiyo baada ya kupitia katika kipindi kigumu cha mauaji ya halaiki.

