Nature

Kagoma Ajazwa Upepo Mechi na Morocco CHAN

TAIFA Stars inaendelea kujifua kujiandaa na mechi ya robo fainali ya michuano ya CHAN 2024 dhidi ya Morocco itakayopigwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, lakini kuna jambo moja limefanywa na Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe kama litafanyiwa kazi basi Stars itavuka.

Kamwe ambaye ni mmoja ya wahamasishaji wa Stars kwa mechi hiyo ya robo fainali alifichua sababu ya kuvaa jezi yenye jina la kiungo wa Simba anayeitumika Stars, Yusuf Kagoma, ni kumtaka afanye kila linalowezekana na wenzake waing’oa Morocco Kwa Mkapa

“Kagoma anapofanya vibaya kila mmoja anazungumza lake mitandaoni, sasa hivyo inamtoa mchezoni, kiukweli nitaandika jezi yangu jina la Kagoma. Asiogope kadi tena na wale Morocco afanye kazi ya kukata kwa sababu kazi ya kiungo wa kati ni kazi kweli kweli sio ya kawaida.

Mbali na hilo, Kamwe amewataka mashabiki kutoihofia Morocco akiamini Stars ina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri. “Kwa mujibu wa takwimu, Stars ndiyo timu iliyoruhusu mabao machache na imetinga hatua hii bila kupoteza mechi yoyote, kwenye tuzo tumebeba zote, kiufupi viwango vya wachezaji wetu ni vikubwa.

Related Posts