Kampuni ya GSM Tanzania Yashinda Tender Ujenzi Uwanja wa Yanga

Kampuni ya GSM Tanzania ( GSM Tanzania Limited ) ambayo ni miongoni mwa Makampuni ya GSM GROUP yanayoongozwa na Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed, imetangazwa Mshindi wa tenda ya kuujenga uwanja wa Club ya Young Africans Sports Club utakaojengwa Makao Makuu ya Yanga JangwaniJijini Dar es salaam.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Mkuu wa Idara ya Habari wa Club hiyo Ally Kamwe amesema Kampuni ya GSM Tanzania ndio iliyoshinda tenda hiyo kwa kuzishinda Kampuni nyingine zilizojitokeza baada ya kukidhi vigezo ambavyo Club ya Yanga iliviweka wakati ilipotangaza tenda hiyo.

Alipoulizwa kuwa ni sifa zipi zilizoifanya Kampuni ya GSM Tanzania kukidhi vigezo hivyo, Kamwe amesema kwa asilimia 100 GSM Tanzania Ltd. imeshinda tenda hiyo kwakuwa hela inayohitajika kuujenga uwanja huo wanayo, uzoefu wa miradi hiyo ya ujenzi wanao na hawahitaji Mtu kati ( middle man ) kukamilisha ujenzi huo tofauti na baadhi ya Kampuni zilizojitokeza ambazo nyingine zilikuwa na Watu wa kati “kwa lugha rahisi walikuja kama Winga’.

“Viongozi wetu wakiongozwa na Rais wa Club walikuwa na ndoto ya kujenga uwanja, wakaamua kuwa uwanja ujengwe Makao Makuu ya Club yetu wakashauriwa na Wataalamu lakini wakagundua lazima wapate nyongeza ya ardhi ili Uwanja wetu ukidhi matakwa CAF, Serikali ikatupatia eneo na hati tunayo na baada ya mchakato huo tukatafuta Mkandarasi ambaye atatujengea uwanja” ——— Ally Kamwe

Related Posts