Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres Atuma Ujumbe Kwa Rais Samia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametuma ujumbe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Desemba 14, 2025, wakati alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo, pamoja na wenzake kutoka Tanzania.

Guterres, amesema Tanzania imekuwa ni rejea muhimu ya amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote na kwamba taswira ya Tanzania kama kielelezo cha amani ilijaribiwa katika uchaguzi wa hivi karibuni uliofanyika Oktoba 29, 2025, ikiwa ni mara ya kwanza kukabiliwa na changamoto hiyo.

“Umoja wa Mataifa ungependa kuona Tanzania inaendelea kubaki katika umoja wake na kuwa mfano bora kwa mataifa mengine,” alisema Katibu Mkuu Guterres alipokuwa akipokea Ujumbe Maalum uliobeba salamu na ujumbe kutoka kwa Rais Samia.

Katibu Mkuu huyo alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo ya kitaifa yenye maana, jumuishi na shirikishi ili kushughulikia chanzo cha matukio ya vurugu yaliyotokea tarehe Oktoba 29, pamoja na kutafuta njia za kudumu za kuyazuia yasijirudie tena.

Aidha, aliahidi msaada kamili wa Umoja wa Mataifa wakati wote na hata baada ya Tume ya Uchunguzi iliyoanzishwa nchini Tanzania kukamilisha majukumu yake.

Related Posts