Nature

Kesho ni Kushambulia tu, Hakuna Kukaa Nyuma – Kocha wa Yanga

Kuelekea mchezo wa marudiano wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Silver Striker Fc ya Malawi utakaopigwa kesho Oktoba 25, 2025, kocha Yanga Sc, Patrick Mabedi amesema wachezaji wake wamejiandaa vizuri na kuna nguvu kubwa, hamasa na ari baina yao.

Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Mabedi amefichua kuwa timu hiyo kesho itakuwa na jukumu la kuambulia tu na sio kukaa nyuma kwa kuwa tayari wapo nyuma kwa goli moja dhidi ya miamba hiyo ya Malawi.

“Kwenye mpira kila mchezo una presha na sisi tunaishi kwenye hiyo presha na tunajua kuna presha kubwa hasa kwa mashabiki wetu lakini jambo la muhimu kwenye mchezo wa kesho nikufanya vizuri na kusonga mbele ili kuondoa hiyo presha na Wachezaji vwote wamejiandaa vizuri na wako tayari kuipambannia nembo ya Klabu yetu” — amesema

“Kesho tunatakiwa kushambulia tu hatutakiwi kukaa nyuma. Tayari wapinzani wetu wako mbele kwa goli moja na tunatakiwa kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho ili tusonge mbele na huo ndo ukweli na wala hakuna njia nyingine” — amesema Mabedi

Related Posts