
Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imepanga Septemba 18, 2025 kuendelea na usikilizaji wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Majaji watatu akiwemo Jaji Dunstan Ndunguru wamepanga tarehe hiyo kusikiliza majibu ya Upande wa Jamhuri kuhusu mapingamizi ya Lissu ya kutaka kesi hiyo ifutwe kwa sababu hati ya mashitaka si halali kutokana na muundo wake.
Pia Lissu ameomba kufutiwa kesi hiyo kwa sababu maelezo ya Mashahidi yamewasilishwa kinyume na sheria, hivyo anaomba ufutwe huo uonevu.
Baada ya kueleza hayo, Majaji wameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18, 2025 kwa ajili ya kuendelea na usikilizaji wa majibu ya Jamhuri kuhusu pingamizi hilo.
Nje ya Mahakama, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dkt.Rugemeleza Nshala amezungumza na Waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa kesi hiyo.
“Ameonyesha kwamba kutokana na uoungofu wa kisheria Mahakama isisite itende haki hiki kinachodaiwa ni uhaini sio badala yake Mahakama imuachie huru baada ya siku 162, Muhimili wa Mahakama ni huru Askari hawana mamlaka ya kuwashika na kuwatoa Watu mahakamani, kama Watu wamejaa taratibu nyingine zifuatwe kitendo cha kuwapiga Watu kinakiuka haki za kiraia na hawa wanaopigwa ni Watu na wana haki kama wao, ndio maana tunapigania muhimili wa Mahakama uwe peke yake na Askari Polisi wake wenyewe,”amesema

