Kutana na Khadija ambaye ni binti mrembo, mwenye heshima na bidii, anatokea Morogoro. Alikuwa ameolewa kwa muda wa miaka miwili, ndoa ambayo mwanzoni ilijaa upendo, maelewano na matumaini ya maisha bora ya baadaye. Hata hivyo, kadri muda ulivyopita, Khadija alianza kukumbwa na changamoto kubwa ambayo hakuwahi kudhani ingeathiri maisha yake ya ndoa—ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa.
Changamoto hiyo ilianza taratibu. Mwanzoni alidhani ni uchovu wa kazi au msongo wa mawazo, lakini hali iliendelea kwa muda mrefu. Alijikuta hana hamasa wala hisia zile alizokuwa nazo awali. Hali hii ilimpa hofu na kumchanganya sana, kwani hakujua pa kuanzia wala nani wa kumweleza. Alijaribu kujifariji kimya kimya, akiamini mambo yangejirudia kawaida, lakini haikuwa hivyo.
Kadri siku zilivyokwenda, ndoa yake ilianza kuathirika. Mume wake alianza kubadilika tabia, kulalamika mara kwa mara, na wakati mwingine waligombana bila sababu ya msingi. Khadija alihisi hatia, huzuni na presha kubwa moyoni. Alianza kujilaumu, akijiuliza kama bado anatosha kama mke au kama kuna tatizo kubwa ndani yake. Amani ya nyumba ikaanza kupotea, hali iliyomuumiza sana kihisia. Soma zaidi hapa
