Kila Timu Itakayoingia Makundi Kombe la Dunia Kupewa Bilioni 25

Taarifa njema kwa Timu zilizofuzu kucheza Kombe la Dunia 2026 [ Timu zote 48 ] , Kila timu itapokea dola za Marekani milioni 1.5 sawa na Bilioni 3 za kitanzania kufidia gharama za maandalizi.

Kama haitoshi kuna gawio la Dola za Kimarekani Milioni 9 sawa na Bilioni 22 za kitanzania ,kwa kila timu iliyopo hatua ya makundi [ Timu zote 48 ] hii ni nje ya Dola milioni 1.5 [ Tsh Biloni 3 ] ya maandalizi

Maana yake Vyama vyote vya Mataifa Washiriki vinapewa kuanzia dola za Marekani milioni 10.5 sawa na Bilioni 25 za Kitanzania kwa kila moja kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya Kombe la Dunia 2026 .

Bilioni Tatu [ za Maandalizi ]
Bilioni 22 [ Mgao hatua ya makundi ]
Jumla ni Tsh Biloni 25 hii ni fedha ambayo kila timu iliyofuzu itapata bila kujali watafuzu hatua inayofuata au vinginevyo

NB : Kadri unavosogea hatua ya juu na dau linaongezeka

Related Posts