
“Taarifa za uhakika zinasema TFF imewaandikia Yanga Princess barua ya kuacha kumtumia mshambuliaji wao kutoka Rwanda JEANINE MUKANDAYISENGA ambaye inasemekana ana maumbile ya kiume, lakini amekuwa akitumika kwenye ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.
Yanga Princess wametakiwa kutomtumia mchezaji huyo kuanzia kwenye michezo ya Ngao ya Jamii hapo tarehe 9/10 dhidi ya JKT, mpaka pale uchunguzi kumhusu utakapokamilika. Inasemekana kuna ushuhuda kutoka kwa watu waliowahi kushiriki naye tendo la ndoa, kuhusiana na kuwepo na uwekano mkubwa maumbile yake kutokuwa ya kike au vinginevyo.
Kumekuwa na changamoto sana kuhusiana na wanamichezo wa kike wenye kiwango kikubwa cha homoni zinazowafanya waonekane wanaume kuliko wanawake, lakini kuna wale ambao wamekuwa na sehemu 2 za siri ile ya kike ambayo ndiyo huwa kama ya asili kwake na ya kiume, wapo ambao sehemu zote ziko active na wale ambao sehemu moja ipo more active. Mambo ya homoni na maumbile yamewasumbua Babra Banda wa Zambia (Kandanda) na Caster Semenya wa Afrika Kusini (riadha).
Kuna masuala ya kanuni na taratibu za kuzingatia kabla ya kufikia maamuzi yoyote, naamini TFF kuna kitu wanakijua zaidi na wamefuata taratibu katika kufikia maamuzi yao. Tuachane na mihemko ya kishabiki bila kuwa na facts.”

