Kivumbi Leo, Dabi ya Yanga na Azam Kutimua Vumbi Leo

Ligi kuu ya soka ya NBC Tanzania bara inaendelea kutimua vumbi leo Machi 15, 2026 kwa mechi mbili huku macho na masikio ya wengi yakielekezwa kwenye pambano la Dabi ya Jiji la Dar es Salaam kati ya Waoka Mitake, Azam FC dhidi ya Mabingwa watetezi, Young Africans Sc katika dimba la Benjamin Mkapa.

Azam FC ndio wenyeji wa mchezo huo wa mkondo wa kwanza baina ya timu hizo kwenye Ligi huku wawili hao ambao ndio timu pekee ambazo hazijaonja ladha ya kufungwa kwenye Ligi mpaka sasa msimu huu wakiangazia kuendeleza rekodi ya ‘unbeaten’ kwenye Ligi.

Yanga Sc ndio vinara wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 35 ambapo ushindi utawasogeza mpaka alama 11 mbele ya Azam FC na Simba SC waliopo nafasi ya tatu na nne mtawalia wakati Azam FC wakitazamia kusogea mpaka alama tano nyuma ya Wananchi ikiwa watachomoza na pointi zote tatu.

Kwenye mechi 12 zilizopita baina ya wawili hao, Yanga imeshinda mara sita, Azam FC mara nne huku wakitoshana nguvu mara mbili na leo Azam ikitegemea ubunifu wa Faisal Salum kama mchei hatari akihusika kwenye magoli 10 ya Ligi msimu huu (magoli 6, asisti 5)

Kwa upande wao Wananchi watahitaji nyota wao Laurindo Dilson ‘Depu’ aendeleze ubora wake mbele ya nyavu za wapinzani baada ya kuchangia magoli saba kwenye Ligi tangu atue klabuni hapo mnamo Januari akifunga magoli sita na kusaidia moja (assist).

20:30 Azam FC Vs Yanga SC
🏟️ Benjamin Mkapa Stadium, Dar

16:00 Mbeya City Vs Singida Black Stars
🏟️ Tanzanite Kwaraa Stadium, Manyara

Related Posts