Klabu ya KMC Fc imethibitisha kuachana na kocha wao mkuu Marcio Maximo
KMC Fc ✍
Tumefikia makubaliano ya kusıtisha mkataba na
Kocha Maximo pamoja na benchi lake la ufundi.
Tunatambua na kuthamini jitihada walizofanya
katika kuboresha utendaji wa timu, ndani na nje ya uwanja, kwa ngazi ya mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla.
Hata hivyo, mabadiliko hayo hayakuweza kuleta matokeo ya haraka, kwani yanahitaji muda wa kutosha ili kuzaa matokeo yanayotarajiwa.
Tunamtakia Kocha Maximo na timu yake kila la heri, na tunabaki wazi kuwatumia tena pindi fursa itakapojitokeza siku za usoni.

