
Klabu ya Singida BS imemuondolea adhabu mchezaji wao Khalid Aucho baada ya kuomba radhi.
Singida BS ✍
Kufuatia barua ya kukiri na kuomba radhi kwa makosa kutoka kwa mchezaji wetu, Khalid Aucho, na baada ya kupitia kwa umakini utetezi pamoja na maelezo yake, Uongozi wa Singida Black Stars kupitia Kamati ya Nidhamu ulikaa na kujadili suala hilo kwa kina.
Baada ya majadiliano hayo, Kamati imefikia uamuzi wa kumuondolea Khalid Aucho adhabu ya kusimamishwa kwa miezi mitatu, kuanzia sasa.
Kwa kuzingatia majuto na dhamira aliyoionesha mchezaji, ameruhusiwa kurejea kikosini na kuendelea kuitumikia timu.
BOOST
Singida Black Stars inaendelea kusisitiza nidhamu, uwajibikaji na weledi kwa watumishi wake wote.
