Kocha Miguel Gamondi Abadilishiwa Majukumu Singida Black Stars

Kutoka kuwa kocha mkuu wa Singida Black Stars hadi kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi ambacho ndio cheo kipya cha Miguel Gamondi ambaye kwa sasa ni kocha wa muda wa Taifa Stars.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi wa Singida BS, leo Jumatatu, Januari 5, 2025 imetangaza mabadiliko katika klabu yao ambapo kocha mkuu wa timu hiyo atakuwa David Ouma.

Kocha Ouma atasaidiwa na makocha wasaidizi Mousa Nd’aw na Muhibu Kanu.

Gamondi amebadilishiwa majukumu na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu, nafasi itakayompa dhamana ya kusimamia mipango ya kiufundi na maendeleo ya jumla ya timu.

Hata hivyo, Singida BS imesema haina pingamizi lolote kwa mamlaka endapo Gamondi atateuliwa kuwa kocha wa kudumu wa timu ya Tanzania, Taifa Stars.

Related Posts