KOCHA WA FAR RABAT AKIRI KUWA PACOME ZOUZOUA NI HATARI
🎙Alexandre Santos Kocha wa Far Rabat aliyeweka wazi Ameondoka na jina la kiungo Pacome Zouzoua, alikiri ni mchezaji huyo ni tishio huku akiulizia kuhusu mkataba alionao Jangwani.
Santos amesema Far Rabat imefungwa na Yanga kutokana na Pacome, aliyekiri wachezaji wa timu hiyo ya Morocco kushindwa kumdhibiti kiasi kwa muda mrefu kutumika kuwarudisha wenyeji mchezoni.
Santos amesema, Pacome ni kiungo hatari akiwa na mpira na kwamba ana uamuzi wa kijasiri mkubwa wa kuufungua ukuta wowote kutokana na ujuzi na ubunifu mpira ukiwa miguuni kwake.

