
Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Angola Pedro Gonçalves kwa sasa akiwa ni Kocha Mkuu wa Yanga SC, amewasilisha rasmi malalamiko yake kwenye Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) dhidi ya Shirikisho la soka la Angola (FAF).
Kocha huyo wa Ureno anadai kuwa Shirikisho hilo limeshindwa kutimiza wajibu wake wa kimkataba, huku akidai kuwa FAF bado ina deni lake la malipo.
Ukimya kutoka FAF na ukosefu wa mpango wa suluhisho umemfanya Gonçalves kutafuta usuluhishi kutoka Shirikisho la soka duniani.
FIFA sasa italazimika kusuluhisha mzozo huu wa kifedha, huku Shirikisho la soka la Angola likikabiliwa na tishio la kuwekewa vikwazo ikiwa ukiukaji wa mikataba utathibitishwa na majaji huko Zurich.
