Nature

KUMEKUCHA: Mahakama Kuu Yafuta Uamuzi wa INEC, Luhaga Mpina Kurudi Kwenye Mbio za Urais Tanzania

Mahakama Kuu, Masijala Kuu-Dodoma, imetengua uamuzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wa kumzuia Luhaga Mpina, mgombea wa urais kupitia ACT-Wazalendo, kurejesha fomu zake za uteuzi. Uamuzi huo umetolewa na jopo la majaji watatu; Abdi Kagomba, Evaristo Longopa na John Kahyoza, ambao wamesema Tume hiyo ilimnyima haki ya kikatiba na haki ya kusikilizwa.

Katika hukumu yao, majaji hao wameeleza kuwa INEC ni taasisi huru na haipaswi kupokea maelekezo kutoka kwa mtu au chombo chochote, ikiwemo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Wamesisitiza kuwa barua ya tume iliyomzuia Mpina haikuwa na msingi wa kisheria na hivyo kubatilishwa rasmi. Aidha, mahakama imeagiza INEC kumpa nafasi mgombea huyo kuwasilisha fomu zake na mchakato wa uteuzi uendelee ulipoishia tarehe 27 Agosti 2025.

Awali, Mpina alikuwa ameondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi wa urais baada ya INEC kupokea pingamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, ikidai hakukidhi vigezo vya kuteuliwa ndani ya chama chake.

Related Posts