Ili kumpata Fei Simba na Yanga walitakiwa kuwa billion 2.1 hapo unalipa billion 1.3 ya kuvunja mkataba Azam na Tsh 800m ya Fei kama hela ya Sign on fee.
Ukitoka hapo lazima Fei umlipe mshahara wa Tsh 80m kwa mwezi hiyo ni kabla ya makato …..fanya Tsh 80m x miezi 12 utagundua kwa mwaka inabidi umlipe Fei mshahara wa Tsh 960m.
Ukichukua 2.1b + 960m utapata kitu kama 3b
Tujiulize Simba na Yanga wamefikia huko ?? Wako tayari kuwekeza 3b kwa mchezaji mmoja kwa mwaka?
Kwenye nchi hii ni Azam pekee wenye huo uwezo,tusilaumiane sana

