
Lavalava amesema amekuwa kwenye Industry kwa muda mrefu na kuna vitu anaweza kuvibaini kama kinacho endelea kwenye game ni mchezo au hiki ni kitu serous. Ameongea hayo kwenye XXL ya Clouds FM hii leo Agosti 25 akitolea ufafanuzi wa andiko lake kuwa ndiye msanii anayeongoza kufanyiwa fitina anapokuwa na kazi mpya, likilenga majibizano ya mtandaoni kati ya Mbosso na Diamond Platnumz kipindi ambacho tayari EP yake iitwayo TIME imeshatoka.
Lavalava anayatazama majibizano ya Mbosso na Diamond kama mchezo tu wa kuharibu sherehe yake (EP ya Time) na ndio maana akachukua muda wa kuwakumbusha ndugu zake kuwa wanavuka mstari.
ALSO READ | Meneja wa Mzize Afunguka, Yanga Wanaroho Mbaya Hawataki Kumuachia Mzize

