Diwani wa Kata ya Goba, Lawrence Mlaki ( @laumlaki ) amechaguliwa kuwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Dar es salaam baada ya kupata kura nyingi za ndio kutoka kwa Madiwani wa Ubungo.
Mlaki ameibuka Mshindi katika Uchaguzi uliofanyika Disemba 2, 2025 katika Ofisi za Manispaa zilizopo Ubungo, Luguruni ambapo mara baada ya kuapishwa Mlaki amesema kuwa wanaenda kubuni vyanzo vya mapato pamoja na kuibua fursa kwa Vijana na kina mama ili waweze kujikwamua na kukua kiuchumi na yuko tayari kuwahudumia Wananchi wa Ubungo kwa nguvu zote.
Aidha hafla hiyo pia iliambatana na kiapo cha Madiwani mbele ya Wananchi waliohudhuria, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Kamati ya Siasa Wilaya ambapo madiwani wametaja vipaumbele muhimu vya kuanza navyo ikiwemo kutatua changamoto za maji, miundombinu mibovu ya barabara na usimamizi wa miradi mipya ya umeme.

