Lengai Ole Sabaya Athamiria Kurudi Tena Kwenye Siasa, Achukua Fomu ya Ubunge
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya leo July 01,2025 ameingia rasmi katika mbio za kulitaka Jimbo la Arumeru Magharibi hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Sabaya kuonekana hadharani katika shughuli ya wazi ya kisiasa, tangu kutoka gerezani kwa kushinda kesi zilizokuwa zinamkabili.
Sabaya ameambatana na Mke wake Jesca Thomas na wamefika katika Ofisi za CCM Wilaya ya Arumeru ambapo Ole Sabaya amekabidhiwa fomu na Katibu wa CCM Wilaya, Camila na alipotakiwa kuongea na vyombo vya habari vilivyopiga kambi ofisini hapo baada ya kupata tetesi kwamba angefika kuchukua fomu, Sabaya ameonekana kutokuwa tayari kuongea akisema “Namuachia Mungu aifanye kazi yake”
Sabaya aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Sambasha iliyopo ndani ya Jimbo hilo na aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Arusha ambapo kwa leo amekuwa Mgombea wa wa 20 kuchukua fomu na kati ya Wagombea hao 20 Wanawake ni watatu.
ALSO READ | Kesi ya Tundu Lissu Yahairishwa Tena, Mwenye Afunguka Kwa Uchungu

