“Mgombea ameshapatikana, na kama nilivyowaahidi…sasa safari ya kuwang’oa na kuking’oa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani..saa nyingine wanajisahau, wanadhani kwamba wanaweza kushinda siku zote, mwaka wa 2025 wanang’oka rasmi madarakani na chama hiki kinaenda kushika hatamu za uongozi”, – Mpina.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina akizungumza mara baada ya kuchaguliwa na Mkutano Mkuu Maalum wa ACT katika nafasi hiyo ya kuwania kuwaongoza Watanzania.

