Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimewateua Wagombea saba kugombea Ubunge Jimbo la Kisesa Mkoani Simiyu akiwemo Lusingi Sitta, Silinde Muachile, Joel Ngowi, Madili Sai, Godfrey Mbuga, Elius Joseph na Gambamala Michael ambapo Mbunge wa sasa wa Jimbo hilo Luhaga Mpina jina lake halijarudi.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ametangaza majina hayo leo July 29,2025.

